Mwaliko wa Kuwasilisha Hadithi Fupi: Kito cha Tungo 2026
Mwaliko wa kuwasilisha hadithi fupi zenye mada huria kwa ajili ya Antholojia ya LEA 2026. Wasilisha hadithi yako kati ya 1 Aprili na 30 Aprili 2026.
MWALIKO WA KUWASILISHA HADITHI FUPI (2026)
Mada: Huria
Idadi ya Maneno: 1,600 hadi 3,300
Idadi ya Hadithi: Moja pekee kwa kila mwandishi
Asili: Ya awali, haijachapishwa
Muundo wa Hati:
Wasilisha hadithi yako kwa faili la Word (.doc au .docx). Kila faili liwe na jina la hadithi na jina la mwandishi. Ukurasa wa kwanza uwe na jina kamili la mwandishi, baruapepe, nambari ya simu na maelezo mafupi ya mwandishi.
Manufaa kwa Waandishi:
Nakala ya kitabu kilichochapishwa
Haki ya kuuza kazi yao
Jinsi ya Kuwasilisha:
Tuma kwa: leapublishers@gmail.com
Kichwa cha Baruapepe: LEA 2026 Antholojia ya Hadithi Fupi
Muda wa Kuwasilisha: Kuanzia 1 Aprili 2026 - 30 Aprili 2026
Gharama: Hakuna malipo yoyote katika mchakato mzima.
Usimamizi:
Mkurugenzi: Onchoka Ongoro (+254703747021)
Mhariri Mkuu Mshauri: Hillary Kaleli Joseph (+254715670426)